CHIRWA ANAHITAJI KIASI HIKI CHA FEDHA ILI ASAINI MKATABA MPYA NDANI YA KLABU YA YANGA.
Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Mzambia Obrey Chirwa
amekanusha tetesi zinazosambaa kuwa anahitaji kiasi cha shilingi milioni
150 ili asaini mkataba mpya na Yanga.
''Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa
ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia, nadhani nia
yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga'', amesema Chirwa.
Aidha Chirwa ameongeza kuwa hapendezwi na maneno yanayoendelea
mitandaoni kuwa amegoma kucheza wakati ukweli unajulikana kuwa ameumia
na bado hajapona ndio mana hajasafiri na timu kwenda Shelisheli.
''Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, mimi
ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya
baadae, niacheni nicheze mpira"ameongeza.
Post a Comment