MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL YAMEUFANYA MSIMAMO KUBADILIKA KUWA HIVI.
Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea tena hii leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kimekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Ruvu Shooting katika dimba la Manungu wakati Tanzania Prisons ikiibuka
na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya.
Kwa matokeo hayo Tanzania Prisons imepanda hadi nafasi ya tano
ikiishusha Mtibwa Sugar, huku Ruvu Shooting ‘Wazee wa kupapasa’ wakizidi
kuchanja mbunga hadi namba saba.
Michezo iliyosalia kukamilisha raundi hii ni vinara wa ligi hiyo timu
ya Simba dhidi ya Mbao wakati Ndanda ikiwa na kibarua kizito cha kuivaa
Yanga SC.
Post a Comment