HII NI REKODI NYINGINE ILIYOWEKWA NA BRAZIL KWENYE SOKA MWEZI FEBRUARY 2018.
Mashabiki wa soka nchini Brazil jana wameshuhudia tukio lisilo la
kawaida michezoni baada ya wachezaji tisa kuoneshwa kadi nyekundu kwenye
mchezo wa 'Derby' kati ya timu za Vitoria na Bahia, baada ya kutokea
vurugu kuelekea mwisho wa mechi.
Vurugu hizo ziliibuka zikiwa zimesalia dakika 11 kabla ya mchezo huo
kumalizika baada ya mchezaji wa Bahia kusheherekea goli akiwa
ameisawazishia bao timu hiyo na kuwa sawa kwa mabao 1 - 1.
Kufuatia bao hilo alilofunga kwa Penati na kushangilia kwa mtindo
ambao ulionekana kuwakera wachezaji wa timu mwenyeji ambayo ni Vitoria
na kuanza kumshambulia kabla ya wenzake wa Bahia kuingilia kitendo
ambacho kilipelekea mwamuzi kutoa kadi hizo na mchezo kuishia dakika ya
79.
Wachezaji sita wa wenyeji wa mchezo Victoria walipata kadi nyekundu
za moja kwa moja huku wachezaji watatu wa timu ya Bahia nao walioneshwa
kadi nyekundu hivyo kufanya mchezo usiendelee.
Refarii alilazimika kuahirisha mechi kutokana na taratibu za mchezo
wa soka kuhitaji angalau wachezaji saba wa timu wawepo uwanjani.
Mahakama ya michezo ya Brazil inasubiriwa sasa kuamua juu ya hatua
gani za kuchukua kufuatia vurugu hizo ambazo zilipelekea kuharibika kwa
mchezo huo ambapo timu zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Post a Comment