DAVID DE GEA AMEINGIA KWENYE REKODI HII BAADA YA MCHEZO WAO NA SEVILLA USIKU WA JANA.

Klabu ya soka ya Manchester United wamerudi nchini Uingereza wakionekana hawana furaha sana baada ya kutoka sare na Sevilla katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán, usiku wa jana (Jumatano) kwenye kombe la klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama Uefa.


Mchezo huo wa kwanza katika hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya ulimalizika kwa sare ya 0-0 huku mlinda mlango wa Manchester United David De Gea akitengeneza rekodi mpya dhidi ya Edwin Van Der Sar.

De Gea alionesha uwezo mkubwa wa kupangua michomo nane ambayo ni idadi kubwa kwa goli kipa wa manchester united kuokoa katika michuano hiyo tangu Edwin Van Der Sar alipofanya hivyo katika mchezo wa fainali dhidi ya Fc Barcelona mwaka 2011.










No comments