MAAMUZI YA FA KWA ROBERTO FIRMINO JUU YA TUHUMA YA KAULI YA KIBAGUZI.
Chama cha soka nchini
England (FA) kimetoa taarifa na kusema kwamba mshambuliaji wa klabu ya
Liverpool Roberto Firmino hana hatia juu ya lugha aliyotumia dhidi ya mchezaji wa Everton Holgate Mason
kutamka maneno ya kibaguzi ndiyo inaelezwa kuleta utata kwa mwamuzi pamoja na Holgate Mason licha ya kuwa Firmino
alitoa maneno hayo kwa kutumia lugha ya
Kireno.
Katika hali ya kawaida
inahitajika utulivu wa hali ya juu pindi linapotea jambo la ubaguzi wa rangi katika nchi
ya England hivyo chama cha soka nchini humo FA kililazimika kumshirikisha
mtaalam wa lugha ya Kireno kwa dhamira ya kutambua maana halisi ya kile
kilichozungumzwa na Firmino.
Dhidi ya mchezaji
mwenzake wa Everton na kugundulika kuwa maana ya maneno au matamshi hayo kwa
mujibu wa mtaalam huyo ameyatambua matamshi hayo hivyo alifuatilia jinsi Firmino
alivyochezesha mdomo wake wakati akiongea na Holgate.
Hata hivyo mtaalam huyo
amesema kwamba ukiangalia jinsi Firmino alivyoongea unaweza kusema kuwa ni mtu mwenye
uzoefu wa kutamka matusi ya ubaguzi wa
rangi katika maisha yake hivyo maneno aliyotamka Firmino kwa mujibu wa mtaalamu
ni kwamba alimwambia Holgate “kaa kimya unajua ni jinsi gani maumivu nimeyapa
nyuma ya mgongo“ alisema mtaalam huyo mara baada ya uchunguzi zaidi.
Ni takribani miezi
miwili sasa imepita baada ya kudaiwa kumtolea kauli ya kibaguzi mchezaji wa klabu
ya Everton inayoshiriki ligi kuu soka nchini England Mason Holgate.
Post a Comment