TIBAR AANIKA SABABU ZILIZO MPELEKA SINGIDA


Mshambuliaji Tibar John amesema sababu iliyopelekea kujiunga na Singida United ni kutokana ni mahali ambapo anaweza kukuza kipaji chake na maslahi pia yamemvutia.

Tibar 19, ambaye amejiunga na Singida jana kwa mkataba wa miaka mitatu amesema anataka kuitumia timu hiyo kama daraja ili kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mshambuliaji huyo alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa msimu lakini amebadili upepo na kujiunga na Walima alizeti hao.

Tibar amekuwa kwenye kiwango bora na timu yake ya zamani ya Ndanda na alikuwa na mchango mkubwa katika kuinusuru na janga la kushuka daraja.

"Nimeichagua Singida kwakua ndio sehemu sahihi ya mimi kuendeleza kipaji changu pia maslahi tuliyo kubalina yamefikiwa," alisema Tibar.

No comments