REKODI MBAYA YA MOURINHO St. JAMES PARK NDIYO SABABU YA UNITED KUPOTEZA LEO.
Klabu ya soka ya Manchester United leo Jumapili Februari 11, 2018
imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini kutoka kwa klabu ya Newcastle
United kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka England.
Goli la Newcastle United limefungwa na Matt Ritchie kunako dakika ya
65 ambapo kwa ushindi huo Mourinho anaendelea kuwa na rekodi mbaya
kunako Uwanja wa St. James Park ambapo hajawahi kushinda mchezo wowote
wa EPL kwenye uwanja huo.
Mourinho akiwa na Manchester United na Chelsea amefanikiwa kushinda
mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi
hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi EFL CUP.
Matokeo ya leo yanaiacha Manchester United ikisalia katika nafasi ya
pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni
kwa pointi 72.
Post a Comment