SARE YA FC BARCELONA INAIFANYA KUWA NA TOFAUTI YA ALAMA HIZI NA ATLETICO MADRID
Klabu ya Barcelona imelazimishwa sare ikiwa nyumbani kwake Camp Nou
dhidi ya klabu ya Getafe kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka nchini Hispania
(La Liga).
Kwenye mchezo huo ambao Barcelona walionekana kuutawala kwa kiasi
kikubwa lakini sio Messi wala Suarez waliofanikiwa kupata goli.
Kwa matokeo hayo Barcelona wanabaki kileleni kwa alama 59 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 52 mapema mchana wa leo Sevilla ilipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Girona inayochezewa na Mkenya Michael Orunga.
Sergio Busquets katika mchezo wa leo dhidi ya Getafe anafikisha michezo 300 ndani ya Laliga akiwa na klabu yake ya Fc Barcelona
Michezo mingine itakayopigwa leo kwenye Laliga ni Valencia vs Levante pamoja na Celta vigo vs Espanyol.

Post a Comment