RONALDO AMESEMA HAFIKIRII MESSI KUWA RAFIKI YAKE HATA SIKU MOJA SABABU YAKE IKO HAPA.
Nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amesema yeye na nyota wa Real
Madrid Criatiano Ronaldo hawawezi kuwa marafiki wala hafikirii kama
itakuwa hivyo baada ya wote kustaafu.
Pamoja na Ronaldo kuwahi kunukuliwa akisema huenda watakuwa marafiki
huko mbeleni, lakini Messi amesema hawana ukaribu hivyo ni ngumu wao
kuwa marafiki.
"Sijui kama tutakuja kuwa marafiki, maana urafiki unajengwa kupitia
kukaa pamoja na kujuana lakini sisi hatuna hiyo nafasi '', amesema.R
Aidha messi amesema wachezaji hao hawana tofauti kila kitu kipo sawa
ila maisha yao hayaingiliani sana kila mtu ana mambo yake na mara nyingi
wanaonana kwenye sherehe za tuzo na kwenye michezo ya El Clasco tu.
Msimu huu Messi amefunga mabao 20 pamoja na kutoa pasi za mwisho 10
kwenye La Liga na Ronaldo amefunga mabao 11 na kusaidia mengine manne.
Post a Comment