AZAM IMESHINDWA KUITOA YANGA NAFASI YA PILI VPL
Klabu ya soka ya Azam FC imelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera
Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliomalizika jioni
hii kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kagera Sugar ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 49 kupitia
kwa Juma Shemvuni kabla ya Azam FC kusawazisha kupitia kwa Idd Kipagwile
dakika 53.
Matokeo hayo ya mchezo wa raundi ya 18 yameiacha Azam FC katika
nafasi ya tatu ikiwa imeongeza alama moja na kufikisha 34 sawa na Yanga
iliyopo nafasi ya pili zikipishana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na
kufungwa.
Kwa upande wa Kagera Sugar imefikisha alama 14 na kuendelea kubaki
katika nafasi ya 15, nafasi moja kutoka mwishoni mwa msimamo. Ligi kuu
itaendelea tena siku ya Jumatano kwa michezo mbalimbali kupigwa.
Post a Comment