SIMBA NA YANGA ZAPANGUA RATIBA YA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA.
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limebadili tena ratiba ya ligi
kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa timu za Simba SC na Yanga SC ambazo
zipo katika michuano ya kimataifa.
Mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United umerudishwa nyuma hadi
tarehe 2 ya mwezi ujao badala ya Februari 4 ilivyo pangwa hapo awali
ambao utachezwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kurudishwa nyuma kwa mchezo huo ni kufuatia klabu ya Simba kupata
nafasi ya kujiandaa na mchezo wake wa michuano ya kombe la Shirikisho
dhidi ya Al Masry ambao unatarajiwa kupigwa Februari 7.
Hasimu wake Yanga SC haitashuka katika dimba la Jamhuri Morogoro
kuikabili Mtibwa Sugar Februari 3 kama ilivyopangwa hapo hawali na
badala yake tarehe ya mchezo huo itatajwa hapo baadaye.
Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara unaonyesha Simba SC inaongoza
kwa kuwa na pointi 45 nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga SC yenye
alama 37 wakati ya tatu ikiwa ni Azam FC yenye jumla ya pointi 35.
Post a Comment