JOHN BOCCO YUPO TAYARI KUWAKABILI AL MASRY DAR ES SALAAM.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa hali ya
mshambuliaji wao, John Bocco inaendelea vizuri na huwenda akacheza
endapo kocha atampatia nafasi hiyo.
Manara ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya mashabiki
wa timu hiyo waliyotaka kufahamu hali ya mchezaji huyo kupitia mtandao
wake wa kijamii wa Instagram.
Niwajuze tu kuwa hali ya Bocco anaendelea vizuri na yupo tayari kucheza kama kocha atampanga.
Miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho cha msimbazi wanao tarajiwa
kurejea hivi punde ni pamoja na mlinda mlango bora wa michuano ya COSAFA
2017, Said Nduda.
Post a Comment