Simba Wamepewa Mapumziko Ya Muda Huu Kutofanya Mazoezi

Kikosi cha vinara wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kimepewa mapumziko mafupi ya siku moja, kutofanya mazoezi baada ya kumaliza mchezo wao wa kimataifa.


Taarifa hiyo imetolewa na uongozi wa timu hiyo mchana wa leo kupitia ukurasa wao maalumu wa facebook huku wakidai wanatarajia kusafiri alfajiri ya kesho kuelekea mkoani Shinyanga.

Kwa upande mwingine, timu ya Simba imerejea katika mashindano ya kimataifa kwa kishindo baada ya kuichapa Gendarmerie ya Djibouti kwa mabao 4-0 katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo uliofanyika (jana) Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


No comments