TAMASHA LA SOKA LA WANAWAKE “LIVE YOUR GOALS” KUFANYIKA FEBRUARI HII MJINI KIGOMA
Tamasha la Soka la wanawake
linalotambulika na Shirikisho la soka uliwenguni FIFA ambalo linafahamika kama
“LIVE YOUR GOALS” linatarajia kufanyika Jumapili ya Februari 25 mesma huu
Mjini Kigoma huku ikienda sambamba na ufunguzi wa Ligi kuu ya wanawake inayofahamika
kama Super 8.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho
la soka nchini (TFF) Salum Madadi amesema, tamasha hilo lenye lengo la
kutoa taswira njema ya soka la wanawake Duniani litashirikisha wakimbizi kutoka
kambi mbalimbali zilizopo kigoma.
"Tamasha hili limepewa jina na
FIFA linaitwa Leave your goal, na linakusudia kutoa taswira njema ya mpira wa
kinamama Duniani, sasa sisi tumepanga kufanyia Kigoma na hili litakiwa la aina
yake kidogo kwa maana tunawashirikisha wakimbizi kutoka kwenye makambi yaliyopo
Kigoma, " amesema.
Madadi amesema Tamasha hilo
limeungamishwa na mambo mengine mawili yakiwemo kozi ya Grassroot ambayo
itaanza kesho na kuhitimishwa siku ya Tamasha hilo huku siku hiyo ya wanawake
yaani Super 8 itakayoanza Februari 24 ikizinduliwa Februari 25 kwa mechi ya
ufunguzi ya Sisters ya Kigoma dhidi ya Simba Queens ya Dar es salaam.
"Tukimaliza Grassroot kwa
watoto tutaanza pilika kwa mechi za wamama ambapo ufunguzi wa Super 8
tunatarajia Mgeni rasmi awe Waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na Michezo
Harrison Mwakyembe, " amesema.
Post a Comment