REKODI YA SIMBA MWAKA 2003 KWA ZAMALEK KUJIRUDIA KWA AL MASRY MJINI PORT SIDE.
Klabu ya soka ya Simba jana imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikishinda kwa jumla ya
mabao 5-0 na sasa itakutana na Al Masry ya Port Side Misri.
Bao moja lililofungwa na Emmanuel Okwi lilitosha kuongeza ushindi wa
Simba baada ya mechi ya kwanza jijini Dar es salaam kushinda mabao 4-0
hivyo kujihakikishia kuvuka hatua ya awali.
Mchezo wa kwanza dhidi ya Al Masry unatarajiwa kupigwa mjini Port
Side ambao ni mji uliopo takribani Kilometa 200 kutoka jiji kuu la Misri
Cairo kati ya tarehe 9, 10 na 11 Machi.
Simba inakumbuku nzuri katika ardhi ya Misri baada ya kufanikiwa
kumtoa nje ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika aliyekuwa bingwa
mtetezi wa michuano hiyo mwaka 2003 timu ya Zamalek.
Katika mchezo wa kwanza mabao ya Simba yalifungwa na Said Ndemla,
John Bocco aliyefunga mawili na Emmanuel Okwi ambaye amefikisha mabao 16
ya kuifungia Simba msimu huu katika mashindano yote
Post a Comment