CAF YAITHIBITISHIA SIMBA KUANZA NYUMBANI DHIDI YA AL MASRY YA MISRI.
Shirikisho la soka Barani Afrika limeithibitishia Simba SC
tarehe rasmi ya michezo yao miwili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya
Misri, ambapo mechi ya kwanza itapigwa Dar es salaam na kisha Simba kwenda
Misri kwa marudiano.
Taarifa ya CAF kwa
vilabu vilivyofuzu kutoka raundi ya awali imeonesha Simba itakuwa dimbani Machi
6 kucheza na wageni wao Al Masry kabla ya Simba kusafiri Machi 16 kwenda mjini
Port Said Misri kwenye mchezo wa marudiano.
Kwa upande wa
klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara amesema wao wameipokea
ratiba hiyo bila shida na imewafurahisha kwasababu wataanzia nyumbani hivyo
watatumia vizuri nafasi hiyo na kushinda mchezo ili kurahisisha kazi nchini
Misri.
Simba imevuka
hatua ya awali baada kuifunga Gendarmerie ya Djibouti kwa jumla ya mabao 5-0
katika mechi mbili ambapo jijini Dar es salaam Simba ilishinda 4-0 na ugenini
jana kushinda 1-0.
Post a Comment