23 WAKIWEMO WACHEZAJI LIGI YA ZANZIBAR WAITWA KUUNDA KIKOSI CHA STARS, MAANDALIZI MECHI ZA KALENDA YA FIFA DHIDI YA ALGERIA A DR CONGO

Kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Moroco ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini Machi 18 mwaajili ya maandalizi ya michezo miwili ya Kalenda ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA).




Kocha Moroco amesema katika kikosi hicho kitakachoanza mchezo wake wa kwanza ugenini dhidi ya Algreria Machi 22 ameongeza wachezaji wanaocheza Ligi ya Zanzibar takribani watatu huku akiongeza kuwa mara baada ya mchezo huo kikosi kitarejea nchini Machi 24 kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa pili dhidi ya DR Congo utakaopigwa Machi 27 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


“Timu yetu ya Taifa itakuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algreria na DR Congo, kikosi kizima kinawachezaji 23 ambapo mara baada ya kuingia kambini Machi 19 kitaanza safari kuelekea nchini Algeria kwa mchezo utakaochezwa Machi 22 na kitarudi Tanzania Machi 24 kujiandaa na mchezo wa pili utakaochezwa Uwanja wa Taifa Machi 27 dhidi ya RD Congo, ” amesema.


Kocha amesema katika uchaguzi wake, hajawaita wachezaji wa Zanzibar kutokana na kiwango walichokionyesha katika mashindano ya CECAFA bali ni kutokana na uwezo wanaouonyesha katika vilabu vyao huku akiongeza kuwa kwa upande wa kiungo Thomas Ulimwengu wamemuita mara baada ya kupata taarifa za Daktari wake zikionyesha kuwa kwa sasa anaendelea vizuri mara baada ya kufanyiwa upasuaji.


Wachezaji walioitwa kambini ni


WALINDA MLANGO:


Aishi Manula
Ramadhan Kabwili
Abdulrahman Mohamed


WALINZI:


Shomari Kapombe
Hassan Kesy
Gadiel Michael


WALINZI WA KATI


Kelvin Yondani
Abdi Banda
Erasto yoni


VIUNGO WA KATI


Hamis Abdallah
Mudathir Yahya
Said Ndemla
Faisal Salum
Abdulahazizi Makame


VIUNGO WA PEMBENI


Farid Mussa
Thomas Ulimwengu
Ibrahim Hajib
Shiza Kichuya
Mohamed Issa


WASHAMBULIAJI


Mwana Samata
Saimon Msuva
John Bocco
Zayd Yahaya
Kikosi cha Taifa Stars

No comments