HALI MBAYA YA HEWA INAVYOENDELEA KUTOA HALI YA TAHARUKI BARANI ULAYA.
Hali mbaya ya hewa imeendelea kuleta taharuki katika eneo kubwa la Bara
la Ulaya, ambapo watu kadhaa kufa na mamia ya nyumba kukosa umeme
kufuatia hali mbaya ya baridi iliyofikia nyuzi joto ya chini ya sifuri.
Nchini Ireland usafiri wa aina mbalimbali pamoja na ule wa ndege
umeahirishwa kufuatia upepo mkali uliosababishwa na dhoruba kali
iliyoziacha nyuma takribani 24,000 na maeneo ya biashara kukosa umeme
wakati nchini Uingereza maelfu wakikumbwa na giza.
Barafu na theluja inayomiminika katika nchi hizo imesababisha hali ya maisha kuwa ngumu kwa wasafari na wananchi kwa jumla.
Tahadhari imeendelea kutolewa kwa wananchi huku kwa wasio na makazi, wakipatiwa hifadhi.
Post a Comment