TAZAMA HAPA NAMNA AMBAVYO ARSENAL WANAVYOGEUZWA KITOWEO KWENYE EPL.
Klabu ya Arsenal imekubali kipigo kingine cha pili mfululizo kwenye
michezo ya Ligi Kuu soka England, baada ya jioni ya leo kukubali kibano
cha goli 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion.
Magoli ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Lewis Dunk na Glenn Murray huku goli pekee la Arsenal likifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang.
Mchezo uliopita Arsenali walikubali kipicgo cha goli 3-0 dhidi ya
wababe wa EPL, Klabu ya Manchester City huku wakipoteza mchezo wa
fainali ya kombe la EFL dhidi ya wababe hao.
Kwenye mchezo huo kama kawaida mashabiki wa Arsenal walikuwa wanaonesha
mabango yaliyosomeka ‘WENGER OUT’ wakimshinikiza kocha wa klabu hiyo
Mzee Wenger kuachia nafasi hiyo klabuni hapo.
Post a Comment