MPANGO MKAKATI WA UONGOZI WA MPIRA WA WAVU NCHINI HUU HAPA.
Uongozi wa Chama cha mpira wa Wavu
nchini kimeandaa mpango mkakati ambao ndio utakuwa dira yao ya kuweza kuukuza
na kuutangaza zaidi mchezo huo ndani na nje ya nchi hususani kwa upande wa
mashindano ya ufukweni na vijana.
Mwenyekiti wa TAVA Meja Jenerali
Mstaafu Patrick Mlowezi amesema, kwa miaka hii minne watakayokuwepo madarakani
wamelenga kuufanya mchezo wa mpira wa Wavu kuwa na nguvu na wenye kupendwa na
kila mtu huku wakilenga pia kuboresha miundombinu ya mchezo huo.
"Kwa miaka hii minne dira yetu
ni kuufanya huu mchezo kukua zaidi hapa nchini lakini tumelenga zaidi kuupeleka
mchezo huu machoni na masikioni mwa watu lakini hatuwezi kufanikisha haya bila
kuwa na viwanja maeneo mbalimbali tukianza na ngazi za mikoa, " amesema.
"Tunahitaji kuukuza huu mchezo
tukianza na mpira wa ufukweni, lakini pia tuwe na vituo vya kukuza vipaji
vya mchezo huu kwa watoto kwani mpaka sasa tunavituo vichache kimoja kipo
Mwanza na kingine Mtwara lakini havina usimamizi mzuri wa mchezo huu, "
amesema.
Mlowezo amesema, wamelenga pia
kushiriki mashindano ya kikanda na Kitaifa pamoja na kuweza kuwa na wadhamini
wa kudumu ambao watawapa uhakika wa kuendesha mashindano yao wenyewe.
Mlowezi amesema, wameandaa
kalenda maalumu ambayo itawawezesha kujua pamoja na kuwataarifu wahusika kuhusu
maandalizi ya mashindano mbalimbali yaliyombele yao.
Post a Comment