MAN UNITED WAMETUPWA NJE NA SEVILLA NYUMBANI TUKUTANE NYUMBANI.
Klabu ya Manchester United imeyaaga mashindano ya klabu bingwa barani
Ulaya kwa kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Sevilla kutoka Hispania.
Sevilla ndio walikuwa wa Kwanza kupata goli kunako dakika ya 73 na 78
kupitia kwa Ben Yedder huku goli la Man United la kufutia machozi
likifungwa na Lukaku.
Baada ya mchezo huo, Kocha Manchester United, Jose Mourinho amesema
kuwa ameyapokea matokeo kwa furaha ingawaje wachezaji wake wanamajonzi.
“Ni kweli Kila mtu ana huzuni lakini Mimi nimepokea matokea kwa
furaha katika kipindi ambacho wachezaji wote wamejawa na huzuni. Kwani
baada ya ushindi wa Liverpool niliwambia wachezaji kuwa kila mechi
inayokuja ni lazima tushinde ili tusonge mbele walijua hilo, na kwa Sasa
tufikirie zaidi mechi zinazokuja matokeo hayawezi kubadilika,”amesema
Mourinho kupitia mtandao wa klabu ya Man United usiku wa Jana baada ya
mchezo kumalizika.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment