TWIGA STARS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MICHUANO YA AFCON.
Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel
za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na
mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake
AFCON 2018 nchini Ghana.
Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8,
2018 jijini Lusaka nchini Zambia.
Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v
Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa
Fainali hizo za Wanawake Afrika.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment