MASHINDANO YA KUOGELEA KUANZA RASMI MARCH 24 JIJINI DAR ES SALAAM.
Mashindano ya Taifa ya mchezo wa
Kuogelea yanatarajia kufanyika Machi 24 na 25 mwaka huu Katika bwawa la Shule
ya IST jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha waogeleaji watakaoshiriki
mashindano ya Jumuiya ya Madola.
Katibu Mkuu wa chama cha kuogelea
nchini (TSA) Ramadham Namkoveka amesema, lengo la kuwaalika waogeleaji
hao ni kuweza kuwaweka fiti kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika Michuano ya
Jumuiya ya Madola itakayofanyika Aprili mwaka huu nchini Australia.
"Mashindano haya ni ya siku
mbili na tumewaalika wachezaji wetu walio ndani na nje ya nchi na hasa wale
watakaoshiriki jumuiya ya madola kuona wamefikia wapi katika upande wa
maandalizi, " amesema.
"Tumeshatuma mwaliko kwa
wachezaji wote na Tarehe 16 itakuwa ndio mwisho wa kithibitisha kushiriki,
kwahiyo tunaimani kabisa mashindano haya ambayo yanafanyika mfululizo yataleta
msisimko kwa washiriki na kuweza kuboresha muda wao zaidi, "
amesema.
Namkoveka ameongeza kuwa katika
mashindano hayo pia watachagua waogeleaji wa kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki
mashindano ya Dunia yatakayofanyika Desemba mwaka huu nchini China.
"Wachezaji watakaofanya vizuri
katika mashindano haya watapata nafasi ya kuteuliwa katika timu ya Taifa
kwahiyo sio kwaajili ya Jumuiya ya Madola, tunamahitaji mengi tunapoandaa
mashindano ya Taifa kwahiyo tunatarajia wachezaji kutoka klabu zote wataweza
kushiriki maahindano haya, " amesema.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza
kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment