YANGA WAMEPANGA KUTUMIA MBINU HIZI ILI KUPATA USHINDI UGENINI DHIDI YA WABOTSWANA.
Klabu ya soka ya Yanga imeondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea
jijini Gaborone nchini Botswana, kwaajili ya mchezo wa marejeano, Ligi
ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.
Yanga inakwenda Botswana ikiwa na rekodi ya kushinda mechi 8
mfululizo za ligi kuu, huku katika michezo yake 11 iliyocheza ndani ya
mwaka 2018 kwenye mashindano yote imeshinda mechi 9 na kutoa sare mechi 1
huku ikipoteza moja dhidi ya Township Rollers.
Katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi ya Machi 17 Yanga inahitaji
kupata ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kujihakikishia nafasi ya
kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Msafara wa mabingwa hao wa Tanzania unaongozwa na viongozi 11 huku
wachezaji watakaokuwa na jukumu la kuibebea Yanga wakiwa ni 20. Morali
ya wachezaji wa Yanga huenda imeongezwa na matokeo ya jana kwenye ligi,
ilipoifunga Stand United mabao 3-1 na kufikisha alama 46 sawa na vinara
Simba.
Endapo Yanga itafanikiwa kuiondoa Township Rollers itaingia kwenye hatua
ya makundi ambapo itajihakikishia kitita cha shilingi bilioni 1.1
kutoka CAF. Kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam Yanga ilikubali
kichapo cha mabao 2-1.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza
kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment