MECHI ZA MAJARIBIO NI CHACHE LAKINI TUPO TAYARI KUPAMBANA NA DR CONGO KUWANIA KUFUZU AFCON 2019 NIGER - WACHEZAJI NGORONGORO HEROES
Mara baada ya kumaliza
michezo yake miwili ya Kimataifa ya Kirafiki, Kikosi cha Ngorongoro
Heroes kimesema japo wamepata maandalizi ya muda mfupi lakini wapo
tayari kwaajili ya kupambana na DR Congo katika mchezo wa kwanza wa
kuwania kufuzu kushiriki Fainali za AFCON U20.
Nahodha wa Kikosi cha
Ngorongoro Heroes Dickson Job amesema, mechi mbili bado hazijatosha
kwaajili ya maandalizi lakini mazoezi na maelekezo ya Kocha yataweza
kuwapa muongozo ili kuhakikisha wanafuzu na kuweza kushiriki AFCON
mwakani nchini Niger.
“Tumejiandaa vizuri na
tupo tayari kwa mechi dhidi ya Congo, kwa mechi mbili kiukweli
hazijatosha lakini inatibidi na hii ni kutokana na kutokuwa na muda
mrefu wa maandalizi ila tunaendelea kujipanga na ninaimani tutafanya
vizuri katika mchezo huo na kusonga mbele zaidi, ” amesema.
Job amewaomba watanzania
kuendelea kuwapa sapoti kama ilivyokuwa katika kikosi cha Serengeti
Boys kwani wanaamini wataweza kuwapa furaha watanzania.
Kwaupande wo washambuliaji
wa Kikosi hicho Muhsin Malima na Abutwalib Msheri wamesema wapo imara
kwaajili ya kuhakikisha wanalitetea pamoja na kulitangaza Taifa
kupitia Soka huku wakiongeza kuwa wanajua wanadeni kubwa kwa
watanzania hivyo watapambana ili kuhakikisha wanafanikisha kile
walichokusudia.
“Mechi tulizocheza ni
kipimo kizuri lwaajili ya maandalizi ya mchezo unaofuata ambao
niwakuwania kufuzu AFCON na tunawaahidi watanzania kuendelea kufanya
vizuri na tunawaomba waendelee kuja kutupa sapoti, ” amesema Muhsin
Malima.
Muhsin amewataka
Watanzania kutokukata tamaa kwani bado wapo imara na wanaendelea
kupambana huku wakitunza mazoezi wanayoyapokea kutoka kwa Kocha na
imani yao ni kuweza kufanya vizuri zaidi katika kila mechi.
“Tunafuata maelekezo ya
Kocha na Kila mchezaji anaijua nafasi yake katika mchezo unaofuata
hivyo tunaamini tutapambana kwaajili ya kuhakikisha tunashinda, ”
amesema Abutwalib Msheri.
Msheri amesema, Kikosi
kilichopo kambini ni mchanganyiko wa Serengeti Boys iliyopita na
wachezaji wengine ambao hawakuwa kwenye kikosi hicho na hapo awali
ilikuwa nguvu kuelewana katika mazoezi lakini kwa sasa wapo pamoja na
wachezaji wote ni wamoja na lengo lao pia ni moja kwani mazoezi ya
Kocha yameweza kuwaunganisha ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Kikosi cha Ngorongoro Heroes |
Post a Comment