KUTINYU ANG'ATA MANENO JUU YA MUSTAKABALI WAKE SINGIDA
Kiungo wa Singida United, Tafadzwa Kutinyu amekataa kufunguka kuhusu mustakabali ndani ya timu hiyo baada ya kuhusishwa na kutaka kutimka kwa 'Walima alizeti' hao.
Azam FC imehusishwa sana na raia huyo wa Zimbabwe ambaye amekuwa na kiwango bora msimu huu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao cha msimu ujao.
Kutinyu aliifunga bao moja katika mchezo wa fainali wa FA waliopoteza kwa mabao 3-2 mbele ya Mtibwa Sugar jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kiungo huyo amesema hayuko tayari kuzungumzia chochote kuhusu mustakabali wake ndani ya Singida ingawa kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka kuli.
"Siwezi kusema chochote kama nitabaki au nitaondoka sijui kitu gani kitatokea mbele," alisema Kutinyu kwa kifupi.
Post a Comment