AZAM YATANGAZA KUACHANA NA HIMID


Klabu ya Azam imetangaza kuachana na nahodha wa wao Himid Mao ambaye ameomba kuondoka kwenda kucheza soka la kimataifa.

Himid amekulia katika timu ya vijana ya Azam na ametumikia kwa uadilifu mkubwa mpaka kuamua kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema nahodha huyo ameuomba uongozi umruhusu kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kitu ambacho wamekiridhia.

"Msimu ujao hatutakuwa na nahodha wetu Himid Mao ametuomba kwenda kucheza soka la kulipwa na uongozi umekubali kumpa ruhusa kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine," alisema Jaffer.

Jaffer amekataa kuweka wazi timu ambayo Himid ataenda kuchezea ingawa taarifa zinasema ni kutoka Afrika Kusini.

No comments