WAOGELEAJI 150 KUSHIRIKI MASHINDANO YA TAIFA KESHO BWAWA LA SHULE YA KIMATAIFA YA TANGANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Waogeleaji takribani
150 kutoka Klabu 12 zilizopo hapa nchini wanatarajia kushiriki
mashindano ya Taifa yatakayoanza kesho na kuhitmishwa Jumapili ya
Machi 25 katika Bwawa la kuogelea la
Shule ya
Kimataifa ya
Tanganyika
jijini Dar es salaam.
“Mashindano haya
pia tutayatumia katika kufuzu kwaajili ya mashindano ya Kimataifa ya
14 yatakayofanyika Hangzhou
nchini China na ambayo tumepata Baraka kutoka FINA, kwahiyo vigezo
vya kuchagua wachezaji pia vipo vingi ambavyo tunaamini vitatusaidia
kuweza kupata wachezaji wazuri zaidi, ” amesema.
Katibu Mkuu wa Chama cha
kuogelea nchini (TSA) Ramadhan namkoveka amesema, katika Klabu hizo
zipo Klabu tatu kutoka visiwani Zanzibar huku akiongeza kuwa
wachezaji waliokuwa nje ya nchi kwaajili ya masomo ambao pia
wanajiandaa a mashindano ya Jumuiya ya Madola wameshawasili akiwemo
nahodha wa timu ya Taifa Hilal Hilal.
“Wachezaji takribani 150
watashiriki mashindano haya kutoka klabu 12 za hapa Tanzania ikiwemo
klabu Tatu kutoka Zanzibar ambazo ni Wahuu, KMKM na JKU pia wachezaji
ambao wapo nje ya nchi kwaajili ya masomo na ambao tunatarajia pia
watashiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola, tayari Nahodha Hilal
Hilal ameshawasili, Sonia Tumiyoto, Colins Saliboko, Philips Partick
na wachezaji wengine wanawasili hii leo, ” amesema.
Namkoveka amesema,
wanatarajia kuwa a waamuzi zaidi ya 40 wanaofahamisha na shirikisho
la mchezo wa kuogelea ulimwenguni (FINA) wakiwemo Khalid Lushaka,
Noel Kihunsi, Samson Makere pamoja na Samson Kimimba.
Namkoveka ameongeza kuwa
katika mashindano ya Taifa pia watapata wachezaji watakaofuzu
kushiriki mashindano ya 14 ya Kimataifa yatakayofanyika Desemba 11
mpaka 16 mwaka huu nchini China.
Post a Comment