TIMU YA TAIFA YA KRIKETI YA WANAUME KUANZA KAMBI MEI MAANDALIZI MICHUANO YA AFRIKA U19 ITAKAYOFANYIKA AFRIKA KUSINI MWAKA HUU
Mara baada ya kupata wachezaji takribani 10 watakaoboresha
kikosi cha Timu ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 19 wa
mchezo wa Kriketi ambacho kinajiandaa na Michuano ya Afrika, Kikosi
hicho kinatarajiwa kuanza kambi mwanzoni mwa Mwezi Mei kikiwa katika
makundi.
Mratibu wa Timu za Taifa za mchezo wa kriketi hapa nchini
Hamis Abdallah amesema, wamefanikiwa kupata wachezaji takribani 10 ambao
watafanya idadi ya wachezaji wa timu hiyo kuwa 24 ambao watakuwa Katika
kambi za mikoani kabla ya kukutana mwezi Juni kwaajili ya Kambi rasmi
ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Afrika kusini kwaajili
ya mashindano hayo yatakayoanza mwezi Agasti mwaka huu.
"Baada ya kumaliza mashindano ya mkoa wanachama ambayo
tuliyaandaa kwaajili ya kutafuta wachezaji ambao watafanya maboresho
kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ambayo itaanza maandalizi ya U19
Afrika, baada ya kuwapata vijana hao tumewapa mapumziko na mwanzoni mwa
mwezi Mei wataanza kambi, " amesema.
![]() |
Kriketi |
Post a Comment