SABABU ZA KOCHA WA NGORONGORO HEROES KUCHAGUA WACHEZAJI 28 BADALA YA 30 KATIKA KIKOSI HICHO HIZI HAPA.



Benchi la ufundi la Timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) limefanya mchujo na kupata wachezaji 28 kati ya 43 waliokuwa kambini kwaajili ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu AFCON U20 itakayofanyika mwakani nchini Niger.


Kocha msaidizi wa Ngongoro Heroes Oscar Milambo amesema, kikosi walichokipata kitacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Morocco lengo likiwa ni kuwaangalia nikwanamna gani wanaweza kujiandaa kwenda kwenye hatua ya kufuzu ambapo mchezo wa kwanza watacheza na DR Congo huku akielezea sababu za kuchagua vijana 28 badala ya 30 kama walivyopanga hapo awali.



"Mara baada ya mchujo tutakuwa na mechi ya Kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya Morocco hapa nyumbani, kwahiyo vijana 28 ndio watakaoendelea na maandalizi ya moja kwa moja na mchezo na Morocco utakuwa wa kwanza kuwaangalia wakishindana na vijana wenye umri sawa na wao ili kuona ni kwamna gani sasa tunaweza kujiandaa, " amesema. 



Kocha Milambo amesema, hapo awali walikuwa na lengo la kubaki na vijana 30 lakini vigezo walivyotumia kutafuta vijana hao ndivyo vilivyochangia kupata vijana pungufu. 



"Kwanini vijana 28 nasio 30? Vigezo tulivyotumia kufanya mchujo havijapatikana kwa wengine ndio maana tumepata vijana hawa 28 na hatukuona sababu ya kulazimisha kuongeza kwasababu kwamuda wa maandalizi tulionao wasingeweza kwenda sawa na kasi ya ubora wa wachezaji hawa 28 waliopatikana, " amesema. 



Oscar amesema, wanaamini kuwa timu hiyo inayoundwa na vijana walioshiriki AFCON U17 itafanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na uzoefu walionao



Kwaupande wake Kocha wa Magolikipa wa Timu hiyo Peter Manyika amesema, kwaupande wake anaimani na walinda mlango watatu waliopatikana katika mchujo huo na kwamuda uliopo wa maandalizi utasaidia kufanya marekebisho ya makosa watakayoyaona ili kuweza kufanya vizuri katika nafasi walionazo.



"Wakati wa mchujo kulikuwa na changamoto lakini tumeweza kupata magolikipa ambao tunaamini ni wazuri na wanafuata maelekezo kwa umakini hivyo tunaamini watafanya vizuri, " amesema.

Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.


No comments