SABABU ZA KUMFIKISHA KAMATI YA MAADILI MAKAMU WA RAIS TFF MICHAEL WAMBURA HIZI HAPA.
Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF inakutana
leo Jumatano Machi 14,2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo
itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura
aliyefikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili.
Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na
Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo
mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa
kufika kwenye Kamati ya Maadili.
Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni
uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama
ilivyorekebishwa mwaka 2015.
Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye
leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma
kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na
barua ya uwakilishi.
Makosa anayoshtakiwa Wambura ni
1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo
hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za
Maadili za TFF Toleo la 2013
2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM
LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu
cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume
na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment