MIPANGO YA MAN CITY KUMSAJILI LIONEL MESII IMEFIKIA PATAMU.
Vinara wa ligi kuu soka nchini England Manchester City kupitia kwa
Mkurugenzi wake wa michezo Ferran Soriano, imeweka wazi kuwa hakuna
uwezekano wa kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi.
"Hakuna
uwezekano wa kumsaini Messi, najua yeye na familia yake wanaishi vizuri
na wanafurahia kuwa jijini Barcelona sehemu ambayo Messi anahitaji kuwa
muda wote'', amesema Soriano.
Soriano ameongeza kuwa Messi amesaini mkataba mpya hivi karibuni na
anaipenda klabu ya Barcelona kwani yeye binafsi anafahamiana vizuri na
Messi hivyo anajua si Man City tu bali hakuna klabu ya kumtoa Messi
ndani ya Barcelona.
Nyota huyo wa Argentina, mwezi Novemba mwaka 2017 alisaini mkataba
mpya wa kuendelea kusalia Camp Nou hadi 2021.
Mkataba huo unajumuisha
kifungu cha timu inayomuhitaji italazimika kutoa kiasi cha Euro milioni
700 zaidi ya Trioni moja.
Messi leo atakuwa dimbani kuiongoza timu yake ya Barcelona kwenye
mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya
Chelsea. Mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment