AZAM KUANIKA JEMBE JIPYA KESHO MCHANA



Zikiwa zimepita siku nne tangu ilipomsajili mshambuliaji Donald Ngoma kutoka Yanga klabu ya Azam imetangaza kuwa kesho watamtangaza mchezaji mwingine waliomsajili.

Tukio hilo litafanyika mbele ya Waandishi wa habari saa 6 mchana katika ofisi za timu hiyo zilizopo Mzizima, Dar es Salaam.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd  amesema mchezaji atakaye tambulishwa ni Mtanzania lakini amegoma kumuweka wazi mpaka hiyo kesho.

"Kesho saa sita mchana katika ofisi zetu za Mzizima tutatangaza usajili wa mchezaji wa pili tuliomsajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano mingine," alisema Jaffer.

Jaffer amesema msimu ujao wamejipanga kufanya vizuri hivyo watafanya usajili mkubwa kutimiza azma hiyo.

Inasemakana mchezaji atakaye tambulishwa kesho ni mlinzi wa kulia wa timu ya Yanga, Juma Abdul.




No comments