LEWANDOWSKI AWAAMBIA BAYERN ANATAKA KUTIMKA


Mshambuliaji wa ​​Bayern Munich, Robert Lewandowski imeripotiwa kuwa amewaambia mabosi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Lewandowski 29, amekuwa na msimu mzuri akiwa kinara wa ufungaji akiweka kambani mabao 29 nakuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga mara sita mfululizo.

Raia huyo wa Poland amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na na klabu za Real Madrid na  ​Chelsea kwa muda mrefu sasa.

Wakala wa mchezaji huyo Pini Zahavi amesema mteja wake anataka kutafuta malisho sehemu nyingine kitu ambacho kimeongeza tetesi za nyota huyo kutaka kutimka.

"Robert anahitaji kupata changamoto nyingine katika maisha yake ya soka, sio kwamba anataka kulipwa pesa nyingi hapana ila klabu zote kubwa duniani zinahitaji mshambuliaji mzuri," alisema Zahavi.

No comments