BOCCO AACHWA, OKWI KUJIUNGA NA TIMU KENYA SPORTPESA SUPER CUP


Nahodha wa timu ya Simba John Bocco 'Adebayor' ameachwa katika kikosi cha wachezaji 18 waliosafiri kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Jumatatu.

Kwa upande wa kinara wa mabao wa timu hiyo Emmanuel Okwi ambaye yupo nchini Uganda kwa ya majukumu ya timu ya taifa ataungana na kikosi huko huko Kenya.

Mshambuliaji mpya Marcel Kaheza aliyejiunga na Simba akitokea Majimaji siku chache zilizopita amejumuishwa katika orodha ya wachezaji wa mabingwa hao kwa ajili ya michuano hiyo.

Mbali na Bocco wachezaji wengine ambao hawajajumuishwa kwenye kikosi hicho ni Laudit Mavugo na Asante Kwasi, Nicholas Gyan na James Kotei ambao wamepewa ruhusa maalum.

Kikosi kamili cha Simba kilicho ondoka asubuhi hii ni makipa Said Mohamed, Ally Salim made Aishi Manula.

Walinzi ni Ally Shomary, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili name Mohamed Hussein.

Viungo ni Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin,Marcel Kaheza, Moses Kitandu, Rashid Juma, Said Ndemla na Haruna Niyonzima

Washambuliaji Shiza Kichuya na
Mohamed Ibrahim.

No comments