SIMBA YAMALIZA KWA SARE, MAJIMAJI YAIFUATA NJOMBE MJI


Mabingwa wa ligi kuu bara timu ya Simba imemaliza msimu wa ligi 2017/18 kwa sare ya bao moja baada ya kubanwa mbavu na Majimaji katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea.

Simba ilitumia idadi kubwa ya wachezaji wa akiba ikiaacha nyota wake wa kikosi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup wiki ijayo.

Matokeo hayo yameifanya Majimaji kushuka daraja ikiungana na Njombe ambayo ilikuwa ya kwanza kushuka.

Mshambuliaji Marcel Kaheza aliifungia Majimaji bao hilo dakika ya sita kabla ya Haruna Niyonzima kuisawazishia Simba kwa mkwaju wa penati dakika ya 45.

Simba ilikuwa na nafasi ya kuondoka na pointi zote katika mchezo kufuatia Niyonzima kukosa penati dakika ya 69.


Matokeo ya mechi zote za ligi kuu zilizpigwa leo

Mtibwa Sugar 0-0 Mbeya City

Lipuli FC 1-2 Kagera Sugar

Prisons 1-0 Singida United

Ndanda 3-1 Stand United

Majimaji 1-1 Simba

Njombe Mji 0-2 Mwadui

Mbao FC 1-1 Ruvu Shooting

No comments