SALAMBA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Mshambuliaji Adam Salamba amejiunga na mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Salamba amekuwa na msimu mzuri akiwa na Lipuli FC katika mzunguko wa pili wa ligi hali iliyopelekea kutakiwa na timu za Azam na Yanga.

Salamba anakuwa mchezaji wa pili kusaini Simba baada ya Marcel Kaheza ambaye alijiunga na mabingwa hao siku chache zilizopita.

Mshambuliaji huyo ameonekana amepiga picha mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji 'MO' muda mfupi baada ya kusaini kandarasi hiyo.

Salamba na Kaheza wanatrajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba watakaoshiriki michuano ya SportPesa Super Cup wiki ijayo nchini Kenya.

No comments