AZAM KUISHUSHIA YANGA KIKOSI CHA MAUAJI
Azam FC imepanga kushusha kikosi kizima katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaofanyika uwanja wa Uhuru saa 2 usiku.
Azam imeuchukulia mchezo huo kwa uzito mkubwa kwakua mshindi wa atamaliza nafasi ya pili katika msimamo na kuwa makamu bingwa.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema wamekuwa kwenye maandalizi ya muda mrefu kuelekea mchezo huo ambao unatajwa kuwa kama fainali.
Jaffer ameongeza kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri na morali ipo juu ingawa watakosa huduma ya walinzi Daniel Amoah na Yakub Mohammed ambao ni majeruhi.
"Benchi la ufundi la Azam chini ya Idd Cheche na Abdul Mingange wamesema watapanga kikosi chao cha kwanza bila kuangalia ubora wa Yanga ili tupate ushindi tuweke heshima ya kumaliza nafasi ya pili," alisema Jaffer.
Yanga ipo nyuma ya Azam kwa pointi tatu na kama itashinda mchezo wa leo watakuwa sawa kwa alama lakini vijana hao wa Jangwani watakuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga hivyo watakaa nafasi ya pili.
Post a Comment