YANGA SASA KUFANYA MKUTANO MKUU JUNI 10



Mkutano mkuu wa wanachama wa klabu ya Yanga sasa utafanyika Juni 10 badala ya Juni 17  iliyokuwa imetangazwa awali.

Awali mkutano ulipangwa kufanyika Juni 17 sasa utafanyika Juni 10 ambapo mahali utakapofanyika itatangazwa baadae pamoja na ajenda.

Mwanzoni kabisa ulipangwa kufanyika Mei 5 lakini kutokana na kuwa na ratiba za michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ilibidi usogezwe mpaka Juni 17.

Sababu ya kurudisha nyuma mkutano huo ni kutokana na ile iliyopangwa awali kuwa huenda ikaangukia sikukuu ya Eid El fitr.

Mkutano huo utajadili masuala mbali mbali ya maendeleo likiwemo la kubadili mfumo wa uendeshwaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda mfumo wa hisa.

Ajenda na sehemu utakapofanyika mkutano huo zitatangazwa kwa wanachama siku chache zijazo ambapo kadi zote mpya (za posta) na zile za zamani zitatumika kikubwa ziwe zimelipiwa tu.

No comments