ZIDANE AJIUZULU KUFUNDISHA REAL MADRID


Meneja Zinedine Zidane ametangaza kujiuzulu kuinoa Real Madrid baada ya kuiwezesha kutwaa taji la ligi ya mabingwa mara matatu mfululizo.

Zidane  45, alijiunga na  Real Madrid Januari 2016 akitokea katika timu ya vijana ya klabu na kuiwezesha kupata mataji manne ya Ulaya ndani ya miaka mitano.

Tetesi za Zidane kutaka kuondoka katika klabu hiyo zilizagaa zaidi baada ya kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ulaya wikiendi iliyopita.

Jumamosi iliyopita Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa fainali uliofanyika Kyiv nchini Ukraine.

No comments