YAMETIMIA! PLUIJM KOCHA MPYA AZAM


Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye klabu ya Azam imemtangaza Hans van Pluijm kuwa kocha wao mpya kuanzia msimu wa 2018/19 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kesho Pluijm ataingoza klabu yake ya Singida United kwa mara ya mwisho kesho katika mchezo wa fainali ya kombe la FA kati ya Singida dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mholanzi huyo amechukua mikoba ya Aristica Cioba raia wa Romania ambaye tayari ameshaondoka nchini kufuatia kushindwa kukidhi mahitaji ya klabu hiyo.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema wameingia mkataba rasmi wa mwaka mmoja na Pluijm na wana amini atawasaidia katika michuano mbalimbali msimu ujao.

"Kwa niaba ya Uongozi wa klabu ya Azam napenda kumtangaza rasmi  Hans van Pluijm kuwa kocha wetu mpya kwa mkataba wa mwaka moja.

"Kesho baada ya mchezo wa fainali ya FA kati ya Singida dhidi ya Mtibwa Sugar tutamchukua Hans moja kwa moja kurejea nae Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha utaratibu," alisema Jaffer.

Kabla ya kujiunga na Singida kocha Hans alikuwa anaifundisha Yanga na kufanikiwa kuipa ubingwa wa ligi  msimu wa 2015/16.

No comments