AZAM KUREJEA MAPEMA KAMBINI KUJIWINDA NA KAGAME


Kikosi cha Azam FC kinatarajia kurejea kambini mapema badala ya tarehe ya awali kutokana na kujiandaa na michuano ya Kagame Cup itakayoanza baadae mwezi huu.

Awali Azam ilitangaza kurejea kambini Julai 3 kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi lakini baada ya taarifa hiyo ratiba yao itabadilika.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema wanasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kama michuano hiyo itakuwepo au la ingawa inasemakana itaanza Juni 29.

"Itabidi tuwaambie wachezaji wetu warudi mapema kutoka likizo kama michuano ya Kagame itakuwepo lakini tutasubiri taarifa kutoka TFF kuthibitisha hilo," alisema Jaffer.

Michuano hiyo itakuwa ya kwanza kwa kocha Hans Van Pluijm aliyejiunga na Azam akitokea Singida United.

Mbali na Pluijm kuonekana kwa mara ya kwanza wachezaji Donald Ngoma na Tafadzwa Kutinyu pia wataonekana kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo.

No comments