SIMBA USO KWA USO NA WABABE WA YANGA


Timu ya Simba itakutana na Kakamega Homeboyz katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kariobangi Sharks kwa mikwaju ya penati 3-2.

Homeboyz iliitupa nje ya mashindano Yanga jana kwa kuifunga mabao 3-1 na sasa watakutana na mabingwa hao wapya wa ligi kuu bara.

Licha ya kuingia nusu fainali Simba haikucheza soka safi kama ilivyotegemewa na wengi kitu ambacho kocha Pierre Lechantre anapaswa kulifanyia kazi haraka.

Kiungo Jonas Mkude ndiye aliyefunga penati ya tano na ushindi iliyoipeleka Simba hatua hiyo ambayo watakutana na Kakamega Homeboyz ambayo iliwatoa Yanga.

Penati nyingine za Simba zilifungwa na Haruna Niyonzima na Erasto Nyoni wakati Mohammed Hussein na Paul Bukaba wakipoteza mikwaju yao huku mlinda mlango Aishi Manula akidaka mbili.

Wawakilishi wengine wa Tanzania, Singida United itacheza na AFC Leopards kesho saa 9 alasiri.


No comments