DROO YA UHAI CUP YAFANYIKA, KUANZA JUNI 9 DODOMA
Droo ya ligi ya vijana ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imepangwa kufanyika leo ambapo michuano hiyo itaanza Juni 9 hadi 21 katika kituo kimoja cha Dodoma.
Ligi hiyo itashirikisha timu zote 16 ambapo kwa siku zitachezwa mbili katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Michuno hiyo itarushwa moja kwa moja ya kituo cha luninga cha Azam TV kama inavyofanya ligi kuu ambapo kwa siku zitapigwa mechi mbili saa 8 mchana ya pili saa 10 jioni.
Bingwa wa michuano hiyo atapata milioni tano, mshindi wa pili milioni tatu, mshindi wa tatu milioni moja
pia kutakuwa na tuzo za mchezaji bora, kipa bora na mwamuzi bora.
Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu (TFF), Clifford Ndimbo amesema maandalizi yamekamilka na timu tayari zimeanza kuelekea mkoani Dodoma.
"Maandalizi yamekamilika na kila kitu kipo sawa, baadhi ya timu zimeshaanza kuelekea Dodoma, waamuzi pamoja na maafisa wa TFF," alisema Ndimbo.
Makundi hayo yamepangwa kama ifuatavyo.
Kundi A
Yanga
Ruvu Shooting
Mbeya City
Mbao FC
Kundi B
Simba
Singida United
Stand United
Njombe Mji
Kundi C
Azam FC
Mtibwa Sugar
Mwadui FC
Majimaji
Kundi D
Tanzania Prisons
Lipuli FC
Kagera Sugar
Ndanda
Post a Comment