MASOUD: SIONDOKI SIMBA LABDA WANIFUKUZE


Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesisitiza kuwa hayupo tayari kuondoka leo wala kesho kwa Wekundu hao kwakua bado ana mkataba nao.

Kauli hiyo imekuja siku saa chache baada ya kuzagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anataka kuachana na Wekundu hao ambapo amezikanusha vikali.

Raia huyo wa Burundi ameshangazwa na taarifa hizo ambazo amezikanusha kwa nguvu kubwa akisema ni uzushi mkubwa.

"Hizo taarifa sijui zimetoka wapi, ni uzushi mtupu, mimi ni kocha msaidizi wa timu ya Simba bado nipo Simba na nitaendelea kuwepo labda wanifukuze," alisema Masoud.

Masoud yupo na kikosi cha Wekundu hao kinacho shiriki michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya ambapo tayari kimetinga nusu fainali.

No comments