DE BRUYNE AMTETEA GUARDIOLA INSHU YA YAYA TOURE


Kiungo Kevin De Bruyne amemtetea Meneja Pep Guardiola kuhusu tuhuma za kumbagua Yaya Toure.

De Bruyne anaamini raia huyo wa Ivory Coast ameshindwa kuelewa sababu za Guardiola kushindwa kumpa nafasi ya kucheza.

"Sijajua sababu ya Yaya kusema vile au alivyoandika nadhani sio kweli au ameongeza chumvi, kama hujapewa nafasi ya kucheza inabidi utafute sababu ya jambo hilo kutokea.

"Tulikuwa na msimu mzuri sana uliopita, mwisho wa siku kocha anafanya maamuzi ya nani anastahili kucheza. Nadhani Yaya hakufiti kwenye mfumo," De Bruyne aliimbia  BBC World Football.

Wakala wa Toure, Dimitry Seluk amesema kiungo huyo yupo tayari kulipwa pauni moja kwa wiki kuchezea moja ya timu sita bora Uingereza ili kumuonyesha Gurdiola kuwa bado yupo vizuri.

"Kuna ofa kutoka nchi mbalimbali juu ya Yaya ambazo wapo tayari kumlipa kiasi kikubwa cha pesa lakini tumeamua kuzikataa ili msimu ujao tumuonyeshe Guardiola kuwa alifanya makosa," Seluk aliiambia Sport24.

No comments