MOROCCO AANZA VIZURI SINGIDA, AIPELEKA NUSU FAINALI SPORTPESA


Kocha Hemed Morroco ameanza vizuri kibarua chake baada ya kuingoza Singida United kuingia nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup inayo endelea nchini Kenya.

Morroco ameiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza akiibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya AFC Leopards baada ya kuchukua mikoba ya Mholanzi Hans van Pluijm.

Kocha huyo alitambulishwa Juni 2 baada ya mchezo wa fainali ya FA kati ya Singida dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Matokeo hayo yanaifanya Singida kukutana na mabingwa watetezi timu ya Gor Mahia katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakaopigwa Ijumaa Juni 8.

Mlinda mlango Peter Manyika Junior aliokoa mkwaju wa penati katika muda wa kawaida na kuifikisha Singida hatua hiyo.

Katika mchezo huo penati za Singida zilifungwa na Shafiq Batambuze, Miraji Adam, Danny Lyanga na Elinywesia Simbu huku Kenny Ally akikosa mkwaju wake.

1 comment:

  1. The first time I played on the Sega Genesis, what was
    The first 군포 출장샵 time I played on the Sega Genesis, what was new 김해 출장마사지 was released, all in one 여주 출장샵 place? What was the last time I played on 경주 출장마사지 the Sega Genesis? 광주광역 출장안마

    ReplyDelete