MINZIRO: KMC HAWAJANIPA HESHIMA NILIYOSTAHILI



Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), Fred Minziro amesema hapajewa heshima aliyostahili kufuatia kuletewa kocha mpya bila kupewa taarifa licha ya kuipandisha daraja.

Mchana wa leo timu ya KMC ilimtangaza Ettienne Nyayiragije kuwa kocha wao mkuu kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2018/19.

Minziro ameiambia Tiktak kuwa uongozi haukumpa taarifa yoyote kuhusu mabadiliko ya benchi la ufundi licha ya kukaa nao muda mrefu na kushangaa ameitwa ghafla asubuhi akaambiwa kuwa mikoba yake ameichukua Ettiene.

"Kitendo cha kuleta kocha mwingine bila kunipa taarifa kimenisonesha sana, nimefanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa lakini nimeshangaa kilichotokea leo.

"Mimi nimeipandisha timu hii baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa misimu minne, nilitegemewa kupewa heshima kubwa lakini ndio kama kilichotokea ila mimi taaluma yangu ni ukocha na maisha ni popote," alisema Minziro.

Kocha huyo ameongeza kuwa wiki ijayo atafanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo ambao unataka kumpa majukumu mengine.

Msimu uliopita Minziro aliipandisha ligi kuu timu ya Singida United lakini akatimuliwa na kibarua chake kikachukuliwa na Mholanzi Hans van  Pluijm kama ilivyotokea leo.

No comments