TFF: MTIBWA IKISHINDA TAJI LA FA ITASHIRIKI SHIRIKISHO AFRIKA MWAKANI



Kaimu Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema endapo Mtibwa Sugar itatwaa taji la FA hii leo mbele ya Singida United itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Shirikisho Afrika msimu ujao.

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu ushiriki wa Mtibwa katika mashindano ya CAF kutokana na kufungiwa mwaka 2001 ingawa 'Wakata miwa' wamekuwa wakikisitiza kuwa adhabu yao ilimalizika.

Kidao amesema kwa sasa Mtibwa kama akishinda ataiwakilisha nchi katika michuano ya Shirikisho Afrika labda kama watapata maagizo mengine kutoka CAF.

"Mpaka sasa hatuna zuio lolote kutoka CAF kuhusu Mtibwa kwahiyo kama watafanikiwa kuchukua ubingwa leo ndio watawakilisha nchi katika kombe la Shirikisho labda kama tutapata maagizo mengine," alisema Kidao.

Fainali hiyo itachezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha saa 9 alasiri huku wadau wengi wakiendelea kumimimika jijini humo kutoka sehemu mbalimbali kuitazama.



No comments