MTIBWA YAITOA NISHAI SINGIDA, YATWAA UBINGWA WA FA
Mtibwa Sugar wametawazwa mabingwa wa michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Singida United mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Mtibwa itaiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Singida walianza kwa kasi mchezo huo lakini Mtibwa walikuwa wa Kwanza kupata bao lililofungwadakika ya 21 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango Ally Mustaph 'Barthez' kabla ya Issa Rashid kuongeza la pili dakika ya 37.
Salum Chuku aliipatia Singida bao la kwanza dakika ya 43 baada ya kupokea pasi ya kiungo Kenny Ally huku bao la pili likifungwa na Tafadzwa Kutinyu dakika ya 69.
Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa alimtoa nje Baba Ubaya kwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano dakika ya 80.
Ismail Mhesa aliifungia Mtibwa bao la ushindi dakika ya 88 baada ya kupokea pasi safi ya Kelvin Sabato.
Kiungo Hassan Dilunga amechaguliwa mchezaji bora wa mashindano wakati Habib Kiyombo akiwa mfungaji bora huku Mhesa akipata tuzo ya mchezaji bora wa mechi 'man of the match'.
Post a Comment